Friday, May 31, 2013

ARSENAL SASA WAINYIMA RAHA KABISAAAAAAA MAN UNITED KATIKA DILI LA FABREGAS

IMEWEKWA MEI 31, 2013 SAA 1:30 ASSUBUHI
KLABU ya Manchester United inaweza kulazimika kutoa fedha nyingi ili kumpata Cesc Fabregas, kutokana na Barcelona kuwa tayari kuwauzia mchezaji huyo Arsenal kwa nusu bei kulingana na makubaliano yao wakati anahamia Nou Camp. 
Inamaanisha Barcelona ingeweza kumuuza kwa Pauni Milioni 70 mchezaji huyo, lakini The Gunners wanaweza kupewa ofa ya kumsajili kwa Pauni Milioni 20, hivyo United lazima wapande dau. 
United ina nia thabitio ya kumsajili kiungo huyo wa Hispania, lakini Arsenal sasa ndio imeshikilia mustakabali wa dili hilo na ndiyo wataamua kama kocha mpya David Moyes atampata nyota huyo au la. 
On the move: Cesc Fabrgeas's future is surrounded in uncertainty with Manchester United keen on the midfielder
Njaini: Cesc Fabrgeas anatakiwa Man United 
Cesc Fabregas
Ilikubaliwa wakati Fabregas anarejea Catalan mwaka 2011, kwamba The Gunners watapunguziwa asilimia 50 akiuzwa. 

Thursday, May 30, 2013

AZAM YASAJILI WATATU WAKIWEMO WAWILI WA UJERUMANI...NI MAKINDA TUPU

Amepandishwa; Mudathir Yahya
Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 31, 2013 SAA 5:25 ASUBUHI
WAKATI Simba na Yanga SC zinakwenda mbio kusajili wachezaji wapya, washindi wa pili mara mbili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wao wamesema hawasajili hata mchezaji mmoja, zaidi watapandisha wachezaji kutoka katika akademi yao.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa ameiambia BIN ZUIBEIRY leo asubuhi kwamba, kocha Muingereza Stewart Hall amesema kwa sasa hakuna umuhimu wa kusajili, zaidi ya kuiangalia timu kwanza katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, unaotarajiwa kuanza Agosti.
Nassor amesema kwamba kocha amewaambia iwapo atagundua kuna mapungufu katika timu katika kipindi cha kuanzia Agosti, ndipo atasajili Novemba katika dirisha dogo.
“Unajua mwakani ndio tutakuwa na haya mashindano ya Afrika (Kombe la Shirikisho). Na pia ndio mbio za ubingwa wa Ligi Kuu (Bara) zinapamba moto. Kwa hiyo mwalimu ameomba hicho ndicho kipindi kizuri kusajili,”alisema.
Hata hivyo, Nassor alisema kwamba kocha amependekeza wachezaji kadhaa wasajiliwe kutoka katika akademi ya klabu hiyo, wakiwemo Mudathir Yahya ambaye yupo na timu ya taifa Ethiopia, kipa Hamad Kadebi na Dissmas ambaye kwa sasa yuko kwenye majaribio Ujerumani.
“Tuna vijana wengi wazuri katika akademi yetu, mwalimu anawapa nafasi sasa. Anaamini timu yake ipo vizuri na hana haja ya kuhangaika kutafuta wachezaji wapya,”alisema Nassor.
Mudathir pia alikuwa kwenye majaribio nchini Ujerumani, akarudishwa nchini kujiunga na timu ya taifa, Taifa Stars kujiandaa kwa mchezo wa kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Ethiopia.

SIMBA SC YATAKA KUSAJILI MKALI KULIKO OKWI

Kifaa cha ukweli; Moses Oloya yuko mbioni kutua Simba SC

Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 29, 2013 SAA 1:15 ASUBUHI
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Moses Oloya (20) yupo katika mazungumzo na na klabu ya Simba SC, ambayo yanaendelea vizuri.
Tayari mshambuliaji huyo wa Saigon Xuan Thanh ya Vietnam amerejea Kampala, Uganda kujiunga na timu yake ya taifa, kwa ajili ya mechi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia.
Kiongozi wa Simba SC yupo Uganda tayari na anaendelea na mazungumzo na kiungo huyo, ambaye aling’ara katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwishoni mwa mwaka jana na kuiwezesha Uganda kutwaa Kombe.
Kiongozi huyo aliyefanikisha usajili wa Mganda mwingine, beki Samuel Ssenkoom wa URA, amefikia sehemu nzuri katika mazungumzo na mchezaji huyo mwenye nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. 
Bila shaka, kama mazungumzo yataendelea vizuri, ndani ya siku mbili Oloya atasaini Simba SC.
Na ikimpata mchezaji huyo aliyezaliwa Oktoba 22, mwaka 1992, akitokea KCC ya kwao, aliyoichezea tangu 2009 hadi 2010, Simba itakuwa imelamba dume.
Oloya ni mchezaji mzuri kuliko Emmanuel Okwi ambaye Simba SC imemuuza Etoile du Sahel ya Tunisia na Desemba mwaka jana, Yanga SC na Azam zote zilijaribu kutaka kumsajili bila mafanikio.
Mwishowe Azam ikaona bora kumsajili Brian Umony, wakati Yanga ilibanwa na nafasi ya idadi ya wachezaji wa kigeni, lakini ikamuweka kwenye orodha ya wachezaji inayoweza kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.

MSIBA WA NGWAIR UPO MBEZI BEACH, TARATIBU ZA MAZISHI ZAANZA

  - 20 hours ago
Marafiki, marehemu Ngwea kushoto na M kulia *Na Mwandishi Wetu,* IMEWEKWA MEI 29, 2013 SAA 1:30 MCHANA FAMILIA ya msanii Albert Mangwea aliyefariki dunia jana nchini Afrika Kusini, imeanza taratibu za mazishi na jioni hii inafanya kikao Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam. Nyota wa Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Ngwair, alifariki dunia jana jioni akiwa nchini Afrika Kusini kutokana na kuzidiwa na matumizi ya dawa za kulevya. Wakati mwili wake unakimbizwa hospitali ya St Hellen Joseph, rafiki yake naye, msanii pia M To Te P alikuwa katika hali mbaya, pia kwa utumiaji wa... more »

SUAREZ ASEMA KUIKATALIA REAL MADRID NI NGUMU, REINA NAYE ASEMA YALE YALE KUHUSU BARCA....LIVERPOOL YABOMOKA


IMEWEKWA MEI 30, 2013 SAA 3:45 ASUBUHI MSHAMBULIAJI Luis Suarez amezua hofu juu ya mustakabli wake katika klabu ya Liverpool baada ya kusema itamuwia vigumu kukataa ofa ya Real Madrid. Suarez, anayetumikia kifungo cha adhabu ya mechi 10 kwa kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, amesema katika mahojiano na kituo cha Redio cha Uruguay analazimika kuondoka kutokana na jinsi anavyoshambuliwa na vyombo vya habari England. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema: "Liverpool wanataka nibaki, lakini ngumu kuwakatalia Real Madrid. [image: Bombshell: Suarez has admitted he w... more »